Thursday, June 17, 2010

JAMANI WADAU MNAMKUMBUKA HUYU BWANAA....


Huyu pembeni yangu anaitwa ALLAIN MULUMBA KASHAMA aka MSTAHIKI MEYA WA JIJI! Alikuwa rapa wa kutegemewa wa bendi ya DAIMOND SOUND enzi hiyo ikitamba na mtindo wao wa Dar es salaam Nkibinda nkoe' yenye maskani yake pale Silent Inn mwenge. Huyu bwana nakumbuka alivyokuwa na maringo na Expensive enzi zake na kuna wakati nilimshuhudia kwa macho yangu ingawa nilikuwa mdogo kiaina akikataa kuchukua elfu 50 alizomwagiwa na mwanamke mmoja mwenye pesa kisa izo pesa zilianguka kwenye sakafu wakati yeye alitaka kutunzwa mkononi, baso zile pesa zote ziliokotwa na wapiga vyombo na yeye HAKUZIGUSA wala kuzisogelea ingawa kwa wakati huo elfu 50 ilikuwa ni pesa nyingi sanaa! Sasa mambo na maisha yamebadilika na ivi sasa bado yupo kwenye muziki akipigia kundi la Diamond Musica la hapa jijini, sasa kwa wadau mnaomkumbuka huyu bwana enzi zake ebu mwageni data zenu tuwasikie...

8 comments:

Anonymous said...

namkumbuka alikuwa bwege tu hajui kuimba wala nini

Mama Jo said...

namkumbuka sana asante kwa kutukumbusha ezni hizo Benny...jamaa alikyuwa na maringo kweli ni kama ulivyosema na alikuwa ana so cuuuute by then...also he was a good rapper...nakumbuka enzi zile mlimani tulikuwa hatuikauki pale Silent Inn kuwasilikilza Diamond Sound...they were soo good jamani..wabnenguaji akina marehemu Diana Aston, Elly ndo wali-revolutionalize sanaa ya buruduni by the....Aisee umenikumbusha enziiii thanks

Mama Jo said...

namkumbuka sana asante kwa kutukumbusha ezni hizo Benny...jamaa alikyuwa na maringo kweli ni kama ulivyosema na alikuwa ana so cuuuute by then...also he was a good rapper...nakumbuka enzi zile mlimani tulikuwa hatuikauki pale Silent Inn kuwasilikilza Diamond Sound...they were soo good jamani..wabnenguaji akina marehemu Diana Aston, Elly ndo wali-revolutionalize sanaa ya buruduni by the....Aisee umenikumbusha enziiii thanks

Hadj Drogba "mwana chelsea" said...

AAH!ALEEE MULUMBA KASHAMA KIUKWELI ALILIKAMATA JIJI ENZI HIZO DALADALA SHILINGI MIA TU UNAFIKA SILENT INN,WIMBO "JEATEU" NDIO ULIMTOA KIJANA AKIWA NA STYLE YAKE YA KUFUNGA NYWELE NYUMBA,HUKU KIONGOZI ELLYSTON ANGAI "LE FARAO"AKIUKAMATA KISAWASAWA MPINI WA SOLO,BASS KULIKUA NA MTU ANAITWA ADOLPHE MBINGA,WAIMBAJI KULIKUA NA RIVA HASSAN "SULTAN",MAREHEMU SUZUKII R.I.P.,JONIKO FLOWER "MAUA",RICHARD MANGUSTINO "TEACHER",KING DODOO LABOUCHE BAADAE ROGER MUZUNGU NAE WAKAMTIA KUNDINI,AAH KAKA THOSE WERE THE DAYS,MZEE RWEGASIRA ALIURUDISHIA CHART MUZIKI WA BENDI BONGO KUPITIA BENDI YAKE HIYO ILIYOZINDULIWA NA LE GRA MOPAO KOFFII ANTONIO CHARLES OLOMIDE LE RAMBOW DU ZAIRE(SASA LE RAMBO DU CONGOO)KAKA JAMAA WALIKUA WAKITOA USAFIRI WA COSTA KUWACHUKUA NA KUWARUDISHA WANAFUNZI WA VYUO KWENDA KUCHEZA KIBINDA NKOI SILENT INN - MWENGE,WE ULIKUA MDOGO BENNY ENZI HIZO,ULIZA MUBA NA BENY HAPO KINONDONI CORNER SALON ZAMANI IKIITWA HIVYO,NOW SIJUI JINA LAKE,ILA BEN NA MUBA WAPO HAPOHAPO SALON TOKA ZAMA HIZO,SALON IKO TRAFIKI LIGHT ZA KAWAWA NA MWINJUMA ROAD,IKITOKEA M/NYAMALA UNAIFACE

PAPAA SHERIE SOUVEREIGN LE TANZANIANE said...

HUYO NI MUSTAHIKI MEYA WA JIJI ALEE MULUMBA KASHAMBA,ALIKUA ANAANZISHA WIMBO ULE JETOU HIVI...SALIIII SALIMA..LIBOSO KAKA BOYEEE BOLINGO KAKA BOYEEE AAH LIBOSO KAKA BOYEEE BOLINGO KAKA BOYEEE,ACHA TU KAKA,HIVI YUKO BENDI GANI HUYU JAMAA KWA SASA,WENYE DATA MSAADA TUTANI

KINYAIYAS ENTERTAINMENT said...

Wadau hivi sasa Alain Mulumba yuko katika Bendi ya Diamond Musica ya jijini Dar! Ben.

Hadj Drogba "mwana chelsea" said...

Wacheza show wa kike enzi hizo za diamond sound walikua wakiongozwa na Salma Abeid "mama lao" huyu alikua mtoto wa kitanga lakini habari zake mpaka mombasa zimefika,kulikua pia mtoto wa kike mwenye mwili mdogo lakini hatari,akiitwa KORANDO "kora mi kora",Diana Aston villa R.I.P.,Huyu LILIAN INTERNET mnaemuona Twanga,yaani we acha tu,uliza sasa mwalimu wao alikua nani,huyo si mwingine bali ni RICHARD MANGUSTINO,ndipo alipopewa jina la teacher,jamaa ndiye aliyewafundisha Marehem Diana na LILII INTERNET KUNENGUA,muulize lilii hapo TWANGA atakwambia mangustino ndio alimtoa.Pia nilimsahau katika safu ya uimbaji yule mwimbaji mwenye ulemavu wa miguu papaa IBONGA KATUMBI "JESUS" Sijui yuko wapi nowadays maskini.

Anonymous said...

yule kilema sio alikuwa anaitwa zola ndoga, yupo sinza maeneo ya mapambano anakaa na jimama moja hivi lilikuwa linafanya mambo ya uigizaji anaitwa gladys chiduo jina maarufu ZIPOMPAPOMPA

Website counter