Thursday, June 10, 2010

ANA KWA ANA NA HARUNA MOSHI 'BOBAN'...

Nikiwa na mshambuliaji wa zamani wa wekundu wa msimbazi SIMBA anayechezea timu ya GELFE IF ya Sweden HARUNA MOSHI 'BOBAN' aliyerejea nchini majuzi kwa mapumziko mafupi na nikamuuliza juu ya ugomvi wake na kocha wa Taifa Starz anayemaliza muda wake Marcio Maximo na akasema kwa yaliyomkuta ameamua kustaafu kuchezea timu ya Taifa na kuwaachia vijana wengine, sasa wadau mnaufahamu uwezo wa kusakata soka wa huyu bwana mnakubaliana nae? maana mie mwenyewe nilimbishia na kumtaka arejee kundini maana timu ya Taifa inawahitaji mapro kama yeye bwanaa...

Kicheko kikuuubwa baada ya maongezi marefu, tukiwa na mzee wa ndefuu FOCUS MAUKI...

1 comment:

Anonymous said...

Tatizo la Macio Maximo ndio hilo ugomvi binafsi na wachezaji anaingiza ktk soka ndio maana mpaka leo timu haina KIPA...kisa hamtaki kaseja bora asepe tu

Website counter