Sunday, October 2, 2011

KUELEKEA JUMAPILI YA KESHO MAKANISANI...


AMANI iwe kwenu enyi waheshimiwa wasomaji wangu. Natumai nyote kwa ujumla wenu, mu wazima kiasi cha kuendelea na shughuli zenu salama ila leo nina mawili matatu, kwa ajili ya hawa wanaovaa mavazi yasiyofaa katika nyumba za ibada.

Jamani katika suala la mavazi ni vyema kufahamu kuwa, kila mahala kuna utaratibu wake wa mavazi wazungu wanauita ‘dress code’. Nguo ya ofisini si sawa na ile inayovaliwa msibani, au ile ya msibani si sawa na ile inayovaliwa kwenye sherehe. Mavazi ya mwalimu si sawa nay ale ya daktari n.k

Mambo haya hayaishii huko, kwani huendelea mpaka kwenye nyumba za ibada. Katika kipindi cha hivi karibuni kumezuka mitindo mipya ya kufanya nyumba za ibada kama sehemu ya kufanyia mashindano ya urembo hususani kwa wanawake.

Sikatai kuwa, kila mmoja wetu anatakiwa kuwa msafi mbele za mungu lakini usafi huu haumaniishi kuvaa suruali za kubana, kuacha baadhi ya maeneo nyeti ya mwili nje ama kuvaa nguo fupi!

Nafahamu kuwa nyote mnaelewa fika mavazi maalum ya kuvaa katika nyumba za ibada na badala yake mnafanya makusudi. Mimi nafikiri huu ni ulimbukeni na wala si vinginevyo.

Naelewa si wengi mnaofahamu athari za nyinyi kuvaa mavazi yasiyofaa hususani mnapoenda sehemu takatifu kama vile kwenye madhabahu ya mungu. Na laiti mngeelewa msingethubutu hata siku moja kuvaa mavazi hayo.Ninapoongelea madhabahu nafikiri kila mmoja wenu anafahamu kuwa ni dini gani hasa ninayoilenga.

Miongoni mwa athari hizo kwanza ni kuwajenga watoto waiokuwa na hofu juu ya muumba wao. Kwani watakuwa wakifuata namna mnavyofanya nyie mliowatangulia na hivyo kuvaa mavazi hayo yasiyofaa kanisani.

Na kwa kawaida ya watoto hawataishia hapo. Kwani kitendo cha kuingia na vimini kanisani vitawatia majaribuni waumini wakiume, jambo litakalosababisha matamanio juu yao. Kwa mantiki hiyo hakutakuwa na mawazo ya mungu tena, ispokuwa utawala wa shetani. Kitakachoendelea hapo hebu pata picha ………

Niseme ukweli kutoka moyoni kuwa, katika hili sina tatizo na waumini wa kike wa madhehebu yote ya dini ya kiislamu.Kwani wao wanaelewa fika namna ya kuvaa wakiwa katika sehemu zao za ibada. Wao hujisitiri hasa kama vitabu vya dini vinavyoamuru. Na kwa kuwa wao hawana utaratibu wa kuchanganyika wakati wa ibada, hili kwao bado sio tatizo sana.

Katika haya mavazi yasiyofaa, ningependa kuwageukia na nyie maharusi hasa wa kike. Ninachoelewa mimi ni kwamba, huwa mnapata mafunzo ya aina mbalimbali kwa muda uisopungua wik moja kabla ya ndoa. Darasa juu ya mavazi yanayofaa siku ya ndoa ni moja wapo ya mafunzo hayo.

Cha kushangaza siku ya ibada ya ndoa, mnakuja madhabauni mkiwa mabega wazi. Hivi huku ni kusahau au dharau?
Hebu muogopeni mungu wenu. Heshimuni nyumba za ibada. Pale sio sehemu ya kuonyeshana mavazi, ni sehemutu ya kukutana kifikra na mungu wako. Hivyo si vibaya ukajiandaa vyema kuingia katika mazingira hayo. Vaa yale yanayaokubalika kwa mungu wako na si vinginevyo.

Hili suala la kuwekewa ’ fashion police’ kwenye milango ya makanisa ni aibu kwa waumini na kanisa kwa ujumla. Kwani hainiingii akilini, eti mwenzenu badala ya kuingia kusali, akae mlangoni kukagua nani kavaa vazi gani?

Badilikeni! Muogopeni mungu wenu, vaeni kama ilivyoamriwa kwenye vitabu vyenu vya dini, Ikiwa mnahitaji mifano angaalieni wahudumu wa kanisa ama masista wanavyovaa, hilo ndilo jibu sahihi la mavazi yanayotakiwa kuvaliwa kwenye nyumba zenu za ibada.

Narudia tena BADILIKENI!

1 comment:

Anonymous said...

beni umeongea kweli sana,makala zako zinakuwaga nzuri saana,endelea kaka.

Website counter