Wakati weye ndugu yangu KAJA.... nani ukiangaikia pesa ya mlo mmoja kwa siku, BINADAMU mwenzetu LIONEL MESSI yuko Barabarani akitembeza MKOKO wake wa bei mbaya huo hapo juu aina ya FERRARI SPIDER 799 wenye thamani ya sh Bilion 1.4 daah...
Huyu DOGO hobbie yake kubwa ni kuendesha Magari pamoja na kucheza Soka la Ufukweni kila anaporudi kwao ROSARIO nchini Argentina...
Ni mfuasi mkubwa wa DIEGO MARADONA na anakiri kwamba alipokuwa mdogo alipania sana kucheza kama Mkongwe huyo wa Soka kwakua nae alibarikiwa kutumia zaidi 'GUU' la kushoto na kuweka 'Nadhiri' moyoni kwamba ni lini atakuja kumwona na kumsalimia Maradona achilia mbali Kumkumbatia kama wanavyoonekana hapo juu, maana hata uso wake unaonyesha kufurahia sana kuwa karibu na mtu wa 'Ndoto' yake kwenye SOKA...
Jamaa ana makaka wawili waitwao RONDRIGO na MATIAS pamoja na dada yake wa pekee aitwae MARIA! Wakati anaanza soka alikumbwa na ugonjwa unaosababisha matatizo katika ukuaji wa mwili uitwao Growth Hormone Deficienty ila wakala wa zamani wa Timu ya Vijana ya Barcelona CARLES REXACH aliamua kuongea na wazazi wa Messi kwamba watamgharamia matibabu yake Ulaya kwa makubaliano ya kuichezea Timu yao ya Vijana baada ya kugundua kipaji chake cha ajabu! Baba yake alikuwa ni Mfua chuma viwandani na mama yake ni Mfanya usafi maofisini ivyo walikuwa 'TAABANI' kiuchumi wkt huo ila kwasasa ni mmoja kati ya wasoka matajiri zaidi Duniani na ni wa pili kulipwa kiwango kikubwa cha mshahara Duniani nyuma ya SAMUEL ETOO wa Cameroon daaah ama kweli soka bwana, sasa sio mwanao anapenda Soka alafu we mzazi humpi ushirikiano wowote utakuwa UMEFELI...
No comments:
Post a Comment