Thursday, September 29, 2011

KWA YALIYOTOKEA ZAMBIA JUZI NI MFANO WA KUINGWA NA VIONGOZI WOTE WA AFRICA...


Huyu ndie Rais mpya wa Zambia Mh. MICHAEL SATA, na hapa ni wakati anaapishwa juzi kushika Madaraka mapya ya kuiongoza nchi hiyo...

Na huyu ndie Rais aliyemaliza muda wake Mh. RUPIA BANDA.
RAIS mpya wa Zambia, Michael Sata aapishwa na kuahidi kupambana na ufisadi na umasikini nchini humo.
Akihutubia baada ya hafla ya kuapishwa, Sata ambaye ni kiongozi wa chama cha cha Patriotic Front (PF) ambaye pia anajulikana kwa umaarufu kwa jina la ‘King Cobra’ ameahidi kupambana na umasikini na ufisadi aliouita kuwa ni maradhi ambayo yanapaswa kupatiwa tiba.

‘King Cobra’, ameapishwa rasmi mjini Lusaka kuwa rais mpya wa nchi hiyo baada ya kushinda katika uchaguzi dhidi ya rais anayeondoka Rupiah Banda.Banda ambaye alikuwa aamini machoni mwake kwa kilichotokea, alitoa hotuba yakukubali matokeo hayo huku akiwa anabubujikwa na machozi mbele ya waandishi wa habari.

“Watu wa Zambia wamezungumza na lazima sote tusikilize," Banda alisema maneno hayo kwa hudhuni huku akiwa anafuta machozi baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.Banda aliongeza kuwa, "Nikizungumza kwa nafsi yangu na chama changu, tunakubali matokeo. Sisi ni chama cha kidemokrasia na hakuna namna nyingine yeyote ile."

Habari zinasema kuwa, chama cha Movement for Multiparty Democracy (MMD) kilichokuwa kinaongozwa na Banda kimekuwepo madarakani nchini Zambia kwa miaka 20.

Sata ambaye anajulikana kwa umaarufu ‘King Cobra’, ni kiongozi wa chama cha Patriotic Front (PF) ambaye ana umri wa miaka 74, baada ya kuapishwa alisema kuwa, wawekezaji wa kigeni wanakaribishwa katika taifa hilo la Afrika lililo na utajiri wa madini ya shaba, ili mradi tu watii sheria za ajira nchini humo.

Sata ana ungwaji mkono mkubwa katika eneo hilo la uchimbaji madini ambapo amewalaumu wakurugenzi wa China kuwatumia vibaya, kuwanyanyasa na kuwapa malipo kidogo wafanyakazi nchini humo.

Zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wa Zambia wanaishi chini ya kipato cha dola mbili kwa siku.Siku ya Alhamisi, kulikuwa na ghasia eneo la Kaskazini lenye migodi zilizofanywa na wanaounga mkono upinzani wakiwa hawana subra na matokeo ya Jumanne.

Matokeo hayo yalitangazwa huku majimbo saba yakiwa bado kura zao kuhesabiwa, lakini maofisa wa uchaguzi wamesema Banda hatoweza kumfikia Sata.Habari katika mitaa mbalimbali nchini humo, zinasema kuwa wasiwasi uliogubika matokeo hayo ulisababisha makelele huku wafuasi wa Patriotic Front wakishangilia ushindi wao.

Maelfu ya watu walifurika nje ya geti lenye ulinzi mkali wakipiga ngoma, wakipiga honi na kupeperusha bendera.

No comments:

Website counter