Wednesday, August 31, 2011

INGAWA NI WAZEE, BOLO YEUNG NA VAN DAMME, KUNA 'KITU' WANATUFUNDISHA...


Jina lake halisi anaitwa YANG SZE ila kwa sie wapenzi wa Sinema za 'MAPAMBANO' tumezoea kumwita BOLO YEUNG! Alizaliwa uko Guangzhou nchini China Tar 3 july 1946. Ni mkongwe katika sanaa za mapigani akiwa ni mtaalamu wa Mitindo yote ya Kung Fu na hata Karate na amejifunza michezo hiyo tangu akiwa na umri wa miaka 9! Wengi wetu tunamkumbuka sana kama ADUI namba 1 wa Mastering woote wa enzi hizo kuanzia Bruce Lee, Check Norris na hata kina Van Damme na enzi hizo kama 'MOVIE' adui sio yeye basi tunaona iyo Movie haina ISHU! Lakini sasa ameezeeka kwa umri wake wa miaka 67 alionao sasa ingawa ukimwangalia kwa umri huo bado anaonekana 'FITI' iyo yoote ni kutokana na mazoezi tu, na kama huamini nenda kwa 'Mdingi' yoyote wa kibongo mwenye umri huo kama hujamkuta anachechemea huku akiwa na magonjwa kibao kuanzia BP mpaka kisukari, kwaiyo hapo AMETUFUNDISHA KITU!

BOLO YEUNG enzi zake akitingisha DUNIA...

Hiki nacho ni chuma cha Pua kilichotingisha Dunia kwenye Sinema za mapigano hususani ya Kung Fu na Karate! Anaitwa JEAN CLOUD VAN DAMME akiwa na jina halisi la Kibelgiji akiwa amezaliwa mnamo tar 18 oct 1960. Mkongwe huyu ana umri wa miaka 52 sasa na ameshaanza kuonekana mzee na hata pilika zake pia kazipunguza ingawa nae mazoezi yamemsaidia kutoonekana amechoka zaidi. Mtaalamu huyu wa Karate ameshaoa na kuacha mara 5 na ana watoto 3 sasa, Christopher, Bianca na Nicholas. Ameshakuwaga Mbwia 'Cocaine' ila akaja akaacha iyo tabia na hivi sasa anaishi nchini Marekani na Familia yake!

VAN DAMME enzi zake akitingisha Sayari kwa Movie zake za kusisimua ila mie naikumbuka Blood Sports bwana 'USIPAIME' ile...

VAN DAMME na BOLO YEUNG walivyokutana kwenye Double Impact, ila sasa chungulia hapo chini walipokutana kama 'MAADUI' hasa kwenye Movie ya BLOOD SPORTS ingawa kwasasa ni marafiki wakubwa...

No comments:

Website counter