Wednesday, August 31, 2011

SHEREHE ZA 'CARNIVAL' ZILIVYOFANA JUZI APA LONDON...


Wajameni hapa mjini London tangu juzi Jumapili kulikuwa na sherehe za Carnival katika eneo la Notting Hill ambako ni tukio la kila mwaka linafanyika muda ambao majira ya Summer yanapoelekea Ukingoni. Tukio hili la watu kufurahi na kufanya kila aina ya starehe ikiwemo kuvuta 'Bangi' hadharani huku Polisi anaona ni mambo ya kawaida mradi tu usilete Vurugu...

Wake kwa Waume hujimwaga barabarani kula 'BATA' kwa mavazi mbalimbali, nami pia sikubaki nyuma atiii, si unamjua 'MBONGO' kwenye Bata tenaa...

Polisi wa huku UK kama hujamchokoza anakuwa rafiki yako kabsaaa, si unaona hata 'Kofia' yake nilimwazima kupigia Picha, je Polisi wa kibongo anaweza kukuvulia Kofia yako eti utake kupigia picha weeeeeeeee....

No comments:

Website counter