Tuesday, August 23, 2011

HAWA NDIO MASTAA WA MOVIE NIGERIA WANAONGOZA KWA UVUTAJI WA SIGARA 'ULIOTUKUKA'...


Mkongwe OLU JACOBS, ambaye mie Binafsi huwa 'namuhusudu' saanaaa kwa uigizaji wake Mahiri...

TONTO DINKE.

SEGUN ARINZE.

RITHA DOMINICK.

INI EDO.

MASTAA wa Nollywood wamejipatia umaarufu mkubwa barani Afrika kutokana na kazi zao ambazo zimekubalika katika nchi nyingi za bara hilo.
Si tu ndani ya Afrika hata Ulaya imewakubali wasanii hao. Lakini kama ilivyo kawaida wasanii hao hawakosi kasoro za nje ya runinga ambazo kwa namna moja zinatokana na kipato, hali halisi au tabia za kuzaliwa.
Tatizo kubwa linalowakabili wasanii wengi wa kike sasa ni uvutaji sigara na ulevi wa kupindukia ambao baadhi ya wachunguzi wa mambo wameeleza kuwa ndio tatizo kubwa linalofanya ndoa zao zisidumu.
Hata baadhi ambao hawajaolewa imekuwa ngumu kupata wanaume wa kueleweka kutokana na kutokuwa na misimamo huku wengi wakidhani kwamba si wanawake sahihi wa kulea familia.
Gazeti moja la Lagos limechapisha orodha ya mastaa wanaovuta sigara kupindukia wakiwemo wanaume huku Toto Dikeh akielezwa kwamba ndiye kinara licha ya matatizo ya ugonjwa wa 'ATHMA' unaomkabili...

No comments:

Website counter