Tuesday, August 23, 2011

Anaitwa PASCAL LOKUA KANZA! Ni mwanamuziki mkongwe kutoka Congo DRC aishie na kufanya Muziki wake nchini Ufaransa kwasasa, Ni mwanamuziki anayezungumza Lugha 5 za Dunia kama vile Kiswahili, Lingala, Kireno, Kifaransa na Kiingereza! Ni mmoja kati ya Wanamuziki wanaoheshimika saanaaa nchini humo hasa kutokana na kusaidia kuibua vipaji vya wanamuziki wachanga nchini Congo. Alizaliwa Mwezi April 1958 huko Bukavu, mji ulio kusini mwa Congo kutoka kwa Baba Mkongo aliyekuwa Baharia na Mama yake ni Mrwanda! Mwaka 1964 familia yake ilihamia katika mji mkuu wa Kinshasa na ndipo Baba yake alipofariki na yeye Lokua kama mtoto mkubwa alipewa Jukumu la kulisha Familia yao iliyokuwa Masikini, ndipo alipochukuliwa na kanisa na hatimaye kuwa kiongozi wa Kwaya na hapo ndipo akapata nafasi ya kusafiri kimuziki sehemu mbali mbali mpaka alipoamua kuweka makazi yake mjini Paris Nchini Ufaransa ambako aliingia mkataba na studio ya Sony na kuanza kutengeneza album zake. Alipoulizwa ni kwanini huwa anapenda kutengeneza Video zake kwenye Mazingira 'DUNI' akajibu kwamba huwa inampandisha 'MORARI' zaidi akifanyia huko kwakua ndio kwao alikokulia! Sasa hiyo apo chini ni VIDEO ya wimbo wake uitwao 'NAKONZONGA' ambao upo katika Albuma yake ya sasa inayotamba Duniani...

No comments:

Website counter