Saturday, May 7, 2011

NAAM SASA ZIJUE SIRI 'KADHAA' ZA KUMJUA MPENZI WAKO 'ALIYEKUSALITI' MUDA MCHACHE ULIOPITA...


KUNA baadhi ya watu wanayatendea haki mapenzi; wapo makini kwa kila kitu katika uhusiano wao na hivyo kuwa kama wanaishi kwenye paradiso ya pekee. Pia, wapo wengine ambao wanayaona mapenzi machungu, wanayachukia na kwa hakika wanalaani kukutana na wenzi walionao.

Kwa nini? Kwa sababu kila siku ni ugomvi, hawana amani. Hawapati muda wa kukaa na kupanga mambo yao, kila wakikutana ni ugomvi. Kunyang’anyana simu na kupekua meseji ndiyo sehemu ya uhusiano wao.

Hawaaminiani. Rafiki zangu, lazima ujue kwamba, katika upande huu ninaozungumzia wa mapenzi ya vurugu kama wanaishi ndani ya tanuru la moto, kuna sababu nyingine nyuma ya pazia. Ipo!
Si nyingine ni USALITI! Utakapoona wapenzi hawaishi ugomvi, ujue kwamba wanaishi kwa mashaka. Kila mmoja haamini kama mwenzake siyo ‘cheche’. Pamoja na ugomvi wao, wengi wanashindwa kuwatambua wenzi ambao wamewasaliti muda mfupi uliopita.

Rafiki zangu, katika mada yetu ya leo, nitakupa siri 10 ambazo ukizizingatia utagundua kama mpenzi wako amekusaliti muda mfupi uliopita. Hapa namaanisha utaweza kumjua mpenzi aliyekusaliti ndani ya saa 24.
Tafadhali weka mawazo yako hapa ili uweze kumgundua mwenzi ambaye ni ‘mwizi’ wa haki yako. Hebu twende tukaone.

RATIBA YA GHAFLA
Rafiki zangu, ukishaanza kuwa na wasiwasi na mpenzi wako kwamba huenda anataka kukusaliti, jambo la kwanza kabisa unalotakiwa kukumbuka ni sehemu aliyokuambia amepitia/anakwenda ilikuwa katika mipango yake au amefanya safari ya kushtukiza?

Hii ni dalili ya kwanza kabla hata hamjakutana nyumbani; “Sorry baby, kuna sehemu napitia mara moja, nitachelewa kidogo kurudi nyumbani,” kauli kama hii iangalie sana.
Mwingine anaweza kupiga simu na kusema: “Mume wangu, bosi ametupa ofa ya dina wafanyakazi wote, kwa hiyo nitachelewa kurudi nyumbani, samahani sana dear.”

Kauli hizo mbili ni alama ya kwanza katika kushibisha hoja yako ya kusalitiwa kama ni kweli atakuwa amefanya hivyo. Kumbuka kwamba, si lazima kila anayesema amepata dharura amesaliti, twende katika hatua nyingine.

ANAKWEPA KUWASILIANA
Mtu huyo ambaye ameshatoa taarifa kwamba amepata dharura, utashangaa hataki kuwasiliana na wewe. Mathalani ukimpigia simu, anaweza asipokee na kama akipokea jibu litakuwa: “Nitakupigia baadaye, samahani sipo sehemu nzuri.”

Unaweza kumwandikia meseji lakini pia asijibu. Wapo wengine vichwa ngumu zaidi, ambao wao kuacha kupokea simu na kujibu meseji si vitu muhimu sana, wanazima kabisa! Ukiona dalili hii, ongeza kwenye orodha yako.

UCHANGAMFU KUPITILIZA
Pamoja na mambo hayo hapo juu, lakini mwenzi huyu akirejea nyumbani, huwa mchangamfu kupitiliza. Ana maneno mengi, anaanzisha mijadala ya ghafla na kuifunga mwenyewe. Atajifanya anataka kufanya mambo mengi kwa ajili yako.

Ahadi zake zinakuwa nyingi za ghafla na nyingi zipo wazi kabisa kwamba si rahisi kuzitekeleza. Alama hii ni kati ya zile 10 zinathibitisha kwamba ndani ya saa 24 umeibiwa ‘mali’ zako.

UPOLE KUPITILIZA
Kinyume cha uchangamfu ni upole, kama mwenzi wako ametoka kimapenzi na patina mwingine kwa ile hofu yake moyoni, anaweza kuwa mpole kupitiliza. Anafanya hivyo kwa lengo la kutafuta huruma.

Hana sababu ya kuwa mpole, lakini anaweza kutumia ngao hiyo, ili maswali utakayomuuliza yawe kuhusu upole na ukimya wake, usahau mambo ya kuhisi kuwa umesalitiwa. Hata hivyo, majibu yake yatakuwa ya mkato sana: “Sijisikii vizuri, siku yangu haikuwa nzuri kabisa leo. Kuna mtu nimetibuana naye ofisini, amenichanganya kabisa.”

Alama hii ni moja ya sababu zitakazokufanya uendelee kumchunguza katika hatua zinazofuata ili mwisho ugundue kuwa umesalitiwa au ni wasiwasi wako tu!

UGONJWA WA GHAFLA
Katika kukwepa usumbufu wa maswali mengi, mwingine huamua kujifanya anaumwa. Atarudi akiwa mkimya kuliko kawaida, ukimwuliza atakujibu kuwa anaumwa. Kama mpenzi wake, anajua wazi kuwa hutakuwa na muda wa kuanza kuhisi usaliti badala yake utamjali na kuuliza hali yake.

‘Mgonjwa’ huyu kwa kawaida huwa haumwi magonjwa ‘siriasi’, sana sana atakuambia hajisikii vizuri, kichwa kinamgonga au moyo unaenda mbio. Ukizungumza kuhusu suala la hospitali atakataa akidai hana hali mbaya sana. Mara nyingi hupenda kukimbilia kitandani, akitaka kupumzika.

Anafanya hivyo kwa sababu anakwepa aibu ya kukutanisha uso wake na wako. Mathalani ukitaka kwenda kumnunulia dawa za maumivu atakujibu: “Nimeshameza panadol baby.” Mwenzi wa aina hii unatakiwa umtilie mashaka, maana inawezekana ametoka kufanya kitu kibaya. Sema mwenyewe umeona eeh, sasa kama na wewe yalishawahi kukutokea kwa 'LAAZIZ' wako yakubidi 'UCHUNGUZE' atii...

1 comment:

Anonymous said...

asante kinyaiyas kwa hii ambari umetushtua wenye ndoa au wapenzi tutalifanyia kazi ubarikiwe kwa hili

Website counter