AINA ZA POMBE NA UFANISI WAKE KWA WATUMIAJI!
1. Pombe za Chimpumu, Dengerua, Kabungusi, Kangara, Komoni, Mbege na Chibuku.
Hupoteza  uwezo wa kufikili wa mtumiajiHuongeza ufanisi wa viungo vya mwili  vilivyo katikati ya miguu ya mtumiaji chini ya kiuno kwa mbele, hivyo  kuongeza uwezekano wa mtumiaji kujiusisha na ngono zisizo salama na  kubaka. Zaidi ya 60% ya kesi zote za kubaka zilizotokana na ulevi  zimehusishwa na utumiaji wa pombe hizi!Hukakamaza misuli ya midomo na  kuongeza ufanisi wa koromeo (voicebox),hivyo si ajabu kuwakuta watumiaji  wa pombe hizi wakipayuka ovyo na kwa sauti za juu kuliko kawaida.
2. Pombe za Pingu na Gongo
Hupunguza  kwa kiasi kikubwa uwezo wa kufikiri wa mtumiajiHuongeza joto la mwili  la mtumiaji kwa kuongeza spidi ya metabolism(metabolic activities),  hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuvua nguo hadharani, ili kupunguza  joto la mwili!Kwa upande wa pombe ya pingu, hii huongeza spidi ya  myeyusho wa chakula(Digestion) na ikitokea mtumiaji hajala kwa muda  mrefu huishia kutapika mpaka nyongo. Baada ya kuongeza spidi ya myeyusho  wa chakula pombe hii hulegeza vifuniko vya mwili (sphincter muscles)  hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuachia kokoo madimba iliyo  rojorojo(uharo wa nguvu na wenye harufu kali)Kwa watumiaji wa lile gongo  litengenezwalo kwa kinyesi cha binadamu(kigamboni ni eneo maarufu kwa  biashara hii), wengi wao huishia Intensive Care Units(ICU), na baada ya  hapo hupelekwa Psychiatric Units(wodi za vichaa), kwani zaidi ya 63% ya  watumiaji wa pombe hii huishia kuwa vichaa kamili!
3. Pombe ya Mnazi
Kiasi  cha ulevi (alcoholic contents) kilichomo katika pombe hii,hushambulia  sehemu ya ubongo wa kati (cerebellum), ihusikayo na kutunza utashi,  hivyo si ajabu kwa mtumiaji wa pombe hii kuishia kuvurumusha matusi ovyo  na kuyumba barabara nzima!Iwapo mtumiaji wa pombe hii hatakuwa  mwangalifu na hivyo kunywa mdudu fulani aitwaye kigoto anayekuwa katika  pombe hii, basi mtumiaji huyo atakuwa mlevi mbwa wa mnazi maishani  mwake!Watu hushauriwa kuviepuka vyoo vilivyotumiwa na walevi wa pombe  hii kwani harufu wanayoiacha huko chooni inahusishwa na kuongezeka kwa  magonjwa ya saratani ya pua na ubongo (nose and cerebral cancer)
4. Pombe ya Ulanzi
Pombe  hii hushambulia viunganishi vya mwili (Body Joints), kwa hiyo asilimia  kubwa ya watumiaji wa pombe hii huishia kulala mabarabarani,vyooni na  sehemu nyingine zisizo za kawaida kwa kushindwa kutembea!
5. Pombe za Bia, Konyagi. Wiski na Wine mbalimbali
Pombe  hizi huongeza hali ya kujiamini kwa watumiaji na pia kuwakumbusha kuwa  hapo zamani za kale, waliwahi kupitia shule,hivyo si ajabu kuwakuta  watumiaji wa pombe hizi wakizoza kimombo na kujihusisha na mijadala  isiyo na kichwa wala miguu punde baada ya kulewa!Pombe hizi hushambulia  sehemu zilizo katikati ya miguu chini ya kitovu kwa mbele ya mtumiaji na  kuzifanya sehemu hizo kuwa imara na zenye nguvu(strong and active) na  hivyo kuongeza uwezekano wa kujihusihsa na ngono zisizotarajiwa na  zisizo salama!
SASA KAZI KWAKO KUPAMBANUA!!! 
 
No comments:
Post a Comment