Wednesday, February 2, 2011

HONGERA ZETU 'LEO TENA' KUFIKISHA MIAKA 7


Nakwambia jambo hili kwa uhakika, hapa nchini kuna watangazaji wengi saanaaaa kuanzia kwenye Radio mpaka kwenye TV mbalimbali, ila ni 'WACHACHE' sana wenye vipaji asilia na waliobaki wengine wanabaki kuuza 'sura' 2 bila watu wengi kuthamini mchango wao kwenye Taaluma hiyo hata kama ameifanya kazi kwa miaka 20, na ukijiona wewe ni mtangazaji ambae unafahamika kwa watu bila hata kijitambulisha basi ujue kazi yako na kipaji chako kinakubalika kwa 'WABONGO' ambao ni 'wabishi' saanaaa kumkubali m2 hata kama anastahili sifa hiyo! Sasa miongozi mwa watangazaji wenye vipaji asilia ni 'bidada' DINNAH MARIOS pichani kushoto ambaye ni mtangazaji wa CLOUDS FM akiongoza kipindi maarufu cha 'LEO TENA' kinachoruka hewani kilasiku kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana, sasa yeye na 'Squad' nzima ya LEO TENA kwa mwezi mzima kuanzia jana wanasheherekea miaka 7 ya kuanzishwa kipindi hicho kilichoasisiwa na Marehemu AMINA CHIFUPA ambaye baadae alikuja kuwa Mbunge wa kuteuliwa kutoka Umoja wa Vijana CCM! Nami nikiwa pia kama mwandishi wa Habari na Mtangazaji nautambua uwezo wa wenzangu hawa katika Tasnia hii na ningependa kuwapongeza Member woote wa LEO TENA walioko apo juu pichani, kuanzia DINNAH mwenyewe, ZAMARADI, HUSNA ABDUL na GEA HABIB kwa kazi yao nzuri na wazidi kupendana wenyewe kwa wenyewe na pia kuwa wabunifu zaidi ili waendelee 'kupeta' kwa Wabongo, HONGERENI SANAAA...

No comments:

Website counter