Wednesday, February 16, 2011

HAYA NI MAMBO 8 USIYOYAJUA KUHUSU DIDIER DROGBA WA CHELSEA YA ENGLAND...


Nadhani wengi mnamfahamu, jamaa anaitwa DIDIER YVES DROGBA TEBILY, ni mshambuliaji nyota wa Timu ya wazee wa 'Darajani' CHELSEA ya England. hAya ni mambo kadhaa usiyoyajua kuhusu uyu 'Mshkaji'. Amezaliwa tar 11 march 1978 kule YOUMOSSOKRO mji uliko kusini mashariki mwa IVORY COAST. 2. Akiwa na umri wa miaka mitano wazazi wake waliacha kazi ivyo walimuomba mjomba ake aitwae MICHAEL GOBA aliekuwa anacheza soka Ufaransa amchukue akaishi nae Ufaransa baada ya hali yao kimaisha kuwa ngumu! 3. Alipenda sana kumsaidia Mjomba ake kusafisha viatu vyake vya Soka huku akimwambia kwamba nae anataka akacheze mpira na watoto wenzake ndipo mjomba ake akatambua kwamba kume nae anapenda kucheza mpira. 4. Ana wadogo zake wawili waitwao JOEL DROGBA na FREDY DROGBA mwenye miaka 18 anayeichezea timu ya LEMANS ambao pia ni wanasoka mahiri wanaocheza soka nchini Ufaransa. 5. Mama yake hupenda kumwita Drogba jina la 'TITO' kutokana na kumpenda aliyekuwa Dikteta wa zamani wa Yugoslavia aitwae JOSIP BROZ 'TITO'. 6. Anapenda sana kula kuku na wali na pia Mahindi yaliochanganywa na Maharage aka 'MAKANDE! 7. Ameoa na mkewe ni raia wa MALI aitwae LALLA DIAKITE ambaye walikutana Paris Ufaransa na wamejaaliwa watoto watatu huku mtoto wake mkubwa aitwae ISAAC akielekea kuwa Mwanasoka ajae kama babake! 8. Mkewe ni muislam wakati yeye Drogba ni Mkatoliki.

Hapa DROGBA akiwa na mkewe LALLA...

2 comments:

Anonymous said...

jambo la 9 : drogba anae dada yake pia wa kuzaliwa nae , anakaa london sehemu ya chelsea, kamnunulia nyumba uko, ameolewa na mkenya, aliyekua anamiliki lincons, ben hukuwai kuijua hiyo pub, bado ulikua hujapanda ndege brother

Anonymous said...

thanks ben kwa kutufahamisha kuhusu drogba. uishi milele

Website counter