
Mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi
MSHAMBULIAJI wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amewataka viongozi wake wasimtafutie sababu kwa kumkata mshahara kwani yeye hafanyi kazi na wao bali kocha Patrick Phiri na Meneja wao Innocent Njovu sio uongozi.
Juzi uongozi wa Simba ulitangaza kumkata asilimia tano ya mshahara wa wachezaji wake wawili Mussa Hassan Mgosi na Adbulharim Humud kwa kosa kufika mazoezini na bila kutoa taarifa kwa kocha wala uongozi wake.
 Mgosi alisema kuwa viongozi wanatakiwa wamuweke wazi kama  kunasheria mpya wameanzisha na wanataka ianzie kwake kwani wanachosema  sio kitu sahihi na hivyo ni njama tu.
Alisema yeye hafanyi kazi  na viongozi bali benchi la ufundi likiongozwa na kocha wao na hamekuwa  akitoa taarifa kwa kocha kila anapokuwa na dharura ila kwa sasa tangu  waanze mazoezi hajawahi kukosa  hata siku moja.
''Sijawahi kukosa  mazoezi hata siku moja ila kunasiku kama mbili hivi nimechelewa kufika  mazoezini, lakini sio kukosa na niliongea na kocha kwa nini  nimechelewa'' alisema Mgosi.
Mgosi aliongeza kuwa tangu waanze  mazoezi hayo hajawahi kuona hata siku moja kiongozi yoyote ameenda  katika mazoezi yao zaidi ya benchi la ufundi hivyo ameshangazwa na kauli  hiyo ya kutaka kumchafua iliwatu wamuone kuwa ni mtovu wa nidhamu. 
Kwa  upande wake hana taarifa yoyote ya yeye kukatwa mshahara kutoka kwa  viongozi wake na katika mkataba wake hakuna kipengele kinachoelezea kuwa  atakatwa.
Pia Mgosi alizungumzia maandalizi ya ligi kuu mzunguko  wa pili kwa upande wake alisema amejiandaa vizuri na anamshikuru Mungu  kwa sasa amepona yale maunivu ya mguu yaliokuwa yanamsumbua.
Alisema  kwa sasa atanachotaka ni kuisaidia klabu yake kutetea ubingwa na  kuwaparaha mashabiki wa timu yake ambao wamekuwa wakisubiri raha hiyo na  kutetea kiatu chake za dhahabu.
Hata hivyo alizungumzia kidogo  mechi zao za kimataifa alisema kuwa wanajua kuwa wanamechi ngumu mbele  yao lakini mawazo yao wamewekea katika mechi ya Morocco ambayo  itawawezesha kucheza na TP Mazembe kama wataifunga na kudhidi kuonga  mbele.
 
No comments:
Post a Comment