Saturday, July 3, 2010

KWA MTINDO HUU TUTAFIKA JAMANII...


Jamani msidhani ni masihara hali hii ipo sehemu kibao vijijini na haswa wamama wajawazito ndio huwa maranyingi wapandishwaga humu kwenye AMBULANCE ya Punda eti wanapelekwa Zahanati kujifungua, na maranyingi huwa hawafiki kutokana na kuwa kuna umbali mrefu kufika, sasa matokeo yake wanajifungulia njiani kienyeji enyeji bila Mkunga kuwepo! Na hata ikitokea bahati wakafika uko Zahanati wataambiwa hakuna dawa yoyote na Mkunga yuko mmoja na tena amepata dharura kidogo ametoka nje ya Zahanati, kwaiyo itabidi atafutwe Mkunga wa jadi aje kuokoa Jahazi la maisha ya mama na mtoto wake mtarajiwa! Na kwa mtindo watoto kibao wameshapoteza maisha mara baada ya kuzaliwa! Sasa kama tunaweza kuigharamia Timu ya BRAZIL kwa bilioni 3, kwanini hizo pesa zisinunuliwe magari ya AMBULANCE yakasambazwa kutoa huduma sehemu za vijijini na pesa zingine zikaboresha zahanati za uko ili vifo visiendelee kutokea? Yaani mie nashangaa sana hali hii, labda wadau mnisaidie kimawazo...

No comments:

Website counter